Kujinasua na Wingu la Kizingiti Angani
Mei 15, 2012

Katika filamu, mashujaa na maadui hurushwa kuelekea mbele baada ya kutokea mlipuko. Hii ni kwa sababu mawimbi makubwa ya nishati ya nguvu, yajulikanayo kama nguvu mtikisiko (shock wave), hutawanywa. Kitu hicho hicho hutokea angani wakati nyota inapolipuka, katika kile kinachoitwa mlipuko wa supanova (supernova explosion).

Nguvu mtikisiko kutoka katika supanova husharabiwa katika mzingo wa nje wa nyota uliojaa gesi na vumbi, ambazo hukimbia kutoka katika nyota kabla ya mlipuko. Nguvu hiyo hupasha joto gesi na kutoa mionzi ya x-ray, ambayo wanaanga wanaweza kuipiga picha kwa kutumia darubini (telescope) maalum zilizopo angani kama picha hii mpya uionayo hapo juu.

Wanaanga wamepiga picha hii ingaayo ya wingu la gesi na vumbi, ambayo ilichukuliwa kwa tofauti ya takribani mwaka mmoja. Kwa kulinganisha picha hizi mbili za x-ray, wanaanga wanafikiri kuwa nguvu mtikisiko hatimaye ilifanikiwa kujinasua kutoka katika wingu. Hii ni mara ya kwanza kwa wanaanga kuwa na uthibitisho wa x-ray unaoonyesha nguvu mtikisiko (shock wave) ikijinasua kutoka katika wingu la kizingiti cha gesi na vumbi angani!

Dokezo

Nguvu mtikisiko hii iliyotokana na mlipuko wa supanova katika picha umeongeza jotoridi la gesi katika hali ya kustaajabisha ya nyuzi joto 100,000,000 Celsius!

This Space Scoop is based on a Press Release from Chandra X-ray Observatory .
Chandra X-ray Observatory

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi