Nyota Yenye Siri
Sep. 5, 2012

Angalia ndani ya chumba ulichomo kama kuna vitu mbali mbali vyenye rangi tofauti tofauti, vitu vyote hivyo unavyoweza kuviona vimetengenezwa kwa vitu vya aina moja ambavyo ni chembe chembe za kemikali. 

Nafikiri utakuwa tayari unafahamu baadhi ya majina ya kemikakali kama dhahabu, oxijeni na shaba ambapo kwa ujumla kuna chembe chembe za kemikali 118 tu zinazojulikana hadi leo. Hii inamaanisha kuwa kila kitu unachokiona katika chumba ulichomo na vyote unavyoviona hapa Duniani vimetengenezwa na viwango tofauti tofauti vya chembe chembe hizi za kemikali na ni chembe chambe hizi hizi 118 tu zinazotengeneza kila kitu kilichopo hapa Duniani! 

Hali ni hivyo hivyo hata kwa vitu vinavyopatikana angani, japo kuna uwezekano wa kuwepo kwa chembe chembe za kemikali zaidi huko angani. Japokuwa hadi sasa wanaanga wanafahamu chembe chembe hizi 118 tu. 

Nyingi ya chembe chembe hizi hutengenezwa ndani ya nyota, ambapo baada ya hapo hutawanywa angani na nyota mpya huzitumia kutengeneza chembe chembe nyingi zaidi za kikemikali. Kwa ujumla kila kizazi kipya cha nyota huongeza chembe chembe za kemikali na haswa wakati nyota mpya zinapotengenezwa. 

Hii ina maana kuwa nyota za zamani kama zinazoonekana kwenye kundi la nyota lilioonyeshwa kwenye picha hazina aina mbali mbali za chembe chembe za kikemikali bali zina chembe chembe za kikemikali za hydrojeni na heliam. Ingawa wanaastronomia wamegundua nyota moja ya ajabu ndani ya kundi hili ambayo ina chembe chembe za kemikali za lithium na wanaastronomia hawafahamu ni kwa njia gani kemikali hii imefika pale! 

Dokezo

Chembe chembe za kemikali mpya bado zinazidi kuvumbuliwa na ya mwisho iligunduliwa mwaka 2010, wakati wanasayansi walipotangaza kuwa wamegundua “ununseptium”. Kama huwezi kulitamka jina hilo usijari kwani hata sisi hatujui jinsi ya kulitamka kwa ufasaha! 

This Space Scoop is based on a Press Release from ESO .
ESO

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi