Na Nguvu Iwe Pamoja Nawe
Dis. 17, 2012

Galaxi hii ya kupendeza katika picha ni sehemu ya mfumo wa galaxi tatu zilizoletwa pamoja na nguvu ya mvutano na zimepewa jina la “Leo Triplet”. Umbo lake la kisahani limeharibiwa na nguvu za uvutano za galaxi nyingine mbili. Je unaweza kuona kuwa umbo lake limeharibiwa? Hii ni kwa sababu galaxi hizi tatu zinavutana.

Nguvu ya uvutano ni kitu ambacho tunakitaja sana tunapozungumza kuhusu astronomia, kwa sababu ina nafasi kubwa katika kuubadilisha ulimwengu. Nguvu ya uvutano ni nguvu inayovuta vitu vyote vyenye uzito na vyenye ukinzani na vingine. Hii ndiyo sababu hatuanguki ingawa Dunia ni duara na tunaishi juu yake. Kutokana na jinsi kitu kilivyo kizito ndivyo nguvu yake ya uvutano inavyoongezeka. Hii ndiyo sababu nguvu ya uvutano katika Dunia ni kubwa kuliko ile ilyopo katika mwezi na pia ni sababu ya watu wanahisi kupungua uzito katika mwezi (mara sita chini ukilinganisha na Duniani!). Hii pia ni sababu inayowafanya wanaanga kuelea katika anga za mbali, mbali kabisa kutoka kwenye sayari na nyota.

Nguvu ya uvutano haifanyi kazi ya kuwaweka watu Duniani peke yake, bali pia hufanya sayari ziweze kuwa katika mfumo wa jua kutokana na nguvu ya uvutano ya Jua. Hufanya gesi, mavumbi na mamilioni ya nyota katika galaxi yetu (Milk Way) kuvutwa na kuwekwa pamoja. Hivyo hata galaxi hazizunguki angani peke yake, kuna makundi makubwa ya galaxi ambayo pia yanavutana. Milk Way ni moja kati ya galaxi 40 katika kundi letu la galaxi! Kundi la Leo Triplet ni dogo zaidi na linajumuisha galaxi tatu tu. Unaweza kuona picha ya kundi lote hapa.

Dokezo

Usichanganye kati ya nguvu ya uvutano na usumaku. Usumaku ni nguvu isiyoonekana na yenye uwezo wa kuvuta vitu, ingawa inafanya kazi kwa baadhi ya maada tuu na ina uwezo wa kusukuma vitu pia.

This Space Scoop is based on a Press Release from Chandra X-ray Observatory .
Chandra X-ray Observatory

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi