Amka na Furaha ni Muda wa Kifungua Kinywa!
Aprili 2, 2013

Wiki chache zilizopita, wanaastronomia waliangalia shimo jeusi (black hole) kwa mshangao sana, baada ya kujitokeza katika magimba na kuanza kujipatia kifungua kinywa. Sio kwa maandazi au kitafunwa kingine bali ni supa-Jupita! Supa-Jupita ni gimba kubwa zaidi ya Jupita (sayari kubwa kuliko zote katika mfumo wetu ws Jua), lakini sio kubwa kutengeneza nyota. Katika kesi yetu ni kubwa mara 30 zaidi. Ili kupata uelewa mzuri Dunia inaweza kuingia ndani ya Jupita mara 1300!

Tukio: kundi la wanaastronomia kutoa European Space Agency walikuwa wamekaa usiku wakiangalia anga, wakati muale usiotarajiwa wa X-ray ghafla ulipokatiza katika vioo vya komputa zao. Walijawa na shauku ya kufahamu muale huu ulitokea wapi na kuanza kutafuta chanzo chake. Ambapo waligundua kuwa unatoka katika kiini cha galaksi unayojulikana kwa jina la NGC 4845. Galaksi hii imechunguzwa mara nyingi, lakini katika usiku huu, ilikuwa ikinga’aa mara 1000 zaidi ya kawaida!

Mwanga wake ulitoka katika sehemu uliyopashwa joto kuzunguka kiini  (shimo jeusi), huku kikiachiana na kuanza kutafuna kitu cha ajabu. Shimo jeusi hili katika kiini cha NGC 4845 linakadiriwa kuwa na uzito wa karibu mara 300 000 zaidi ya ule wa Jua letu. Pia hupenda kucheza na chakula chake: kwa muda wa miezi 2-3, lilikuwa linacheza na kitu hiko cha ajabu kabla ya kukitafuna kuwa moja ya kumi ya ukubwa wake wa awali!

Unaweza kuona jinsi tukio hilo lilivyotokea, kama lilivyotengenezwa kwa  komputa hapa

Dokezo

Kuna mipaka maalum inayozunguka shimo jeusi iitwayo event horizion. Ni katika sehemu hizo ambapo kila kitu, hata mwanga ni lazima viiingie katika shimo jeusi. Hakuna kutoroka mara baada ya kuvuka event horizon!

This Space Scoop is based on a Press Release from ESA .
ESA

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi