Kimondo Chaimwagia Maji Jupita
Aprili 25, 2013

Jupita (Sumbula) ni sayari kubwa ya gesi na pia ni sayari kubwa kuliko zote katika mfumo wetu wa Jua, ina uzito wa asilimia 70% ya uzito wa sayari zote zikijumuishwa. Wanasayansi walipooiita Sumbula kama ni sayari kubwa ya gesi, hawakuipa sifa ya uongo kwani kama ukishuka na parashuti katika uso wa Jupita, unaweza usiguse ardhi ngumu. Katika maelfu ya kilometa unaweza ukawa unakatiza katika tabaka la hewa zito lenye dhoruba, kabla ya kufikia katika uso wa kushangaza wa sayari hiyo wenye bahari (ocean of exotic fluid) ya kina cha kilometa 40,000!

Lakini maji haya ya ajabu ambayo mara nyingi yameundwa na haidrojeni sio bahari pekee iliyopo katika Sumbula. Picha hii inaonyesha ramani ya maji katika tabaka la hewa la sayari hiyo iliyotengenezwa na wanaastronomia! Ambapo waligundua kuwa karibu maji yote yaliletwa na chanzo cha kutoka nje, Kimondo cha Shoemaker-Levy 9 ambacho kiliigonga sayari hiyo mwaka 1994. Mgongano ambao ulikuwa wa kustaajabisha! Wakati kimondo hiki cha barafu kilipokuwa kinaingia katika tabaka zito la gesi na ukungu la Sumbula, kilitengeneza shimo kubwa jeusi, lenye kipenyo cha km 6,000 ambalo lilikuwa linaweza kuonyesha uso wa sayari katika picha na 2. Hiki hakikuwa kitu pekee kilichoachwa na kimondo cha Shoemaker-Levy; vimondo vingi hubeba kiasi kikubwa cha barafu katika viini vyake, na kwa hiki hakikuwa tofauti.

Kwa kutumia darubini ya angani ya Herschel, wanaastronomia wametengeneza ramani yenye pande tatu ya maji katika Sumbula, ambapo wingu la blue linaloizunguka sayari hiyo katika picha ni maji. Kuwepo kwa maji katika Sumbula sio jambo la kushangaza sana, lakini ramani inaonyesha kuwa maji mengi yanapatikana katika kizio cha kusini. Hii iliwashangaza wanaastronomia kwa sababu kama maji yalitoka ndani ya sayari basi walitegemea maji yatawanyike sawa katika pande zote. Kujirundika huku kwa maji katika sehemu moja kunaleta hitimisho moja tu: maji yaliletwa na kimondo cha Shoemaker-levy 9 tu! 

Dokezo 

Labda kuna kiini kigumu ambacho ni mara kumi kwa ukubwa zaidi ya Dunia kilichopo katikati ya Sumbula, lakini nguvu ya mkandamizo na joto kali vinaweza kukuzuia kufika karibu yake. Hali katika kiini cha Sumbula ni ya kutisha, jotoridi likiwa juu zaidi ya lile la uso wa Jua na nguvu ya mkandamizo ikikaribia milioni 40 zaidi ya mkandamizo wa hewa Duniani! 

Space Scoop hii imetokana na taarifa kwa vyombo vya habari vya ESA

 

Dokezo
This Space Scoop is based on a Press Release from ESA .
ESA

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi