Sayari Nyeusi Inayofyonza Mwanga
Sep. 15, 2017

Habari njema kwa mbwa mwitu, wanyonya damu na viumbe wote wanaopenda usiku – sayari nyeusi imevumbuliwa! 

Dunia hii mpya ni “sayari iliyo nje ya mfumo wa Jua” ikimaanisha kuwa inazunguka nyota nyingine iliyo nje ya mfumo wetu wa Jua. Hadi sasa, tumegundua Zaidi ya sayari 3500 zilizopo nje ya mfumo watu wa Jua, na baadhi ya sayari hizo ni za kushangaza sana.

Kuna dunia zilizosambaratishwa na nyota zinazozinguka, na nyingine zinazopambana na upepo mkali unaovuma katika mwendo wa maelfu ya maili kwa saa. Moja kati ya sayari hizi zilizo mbali, imefunikwa na uso wa barafu linalowaka!

Hii inaonyesha kuwa, sayari zenye bahati katika Ulimwengu ni zile zenye sifa kama ya Dunia yetu.

Je, ni kwanini tumepata shauku kuhisiana na sayari hii nyeusi ya kipekee? Ni kwa sababu inashangaza kwamba tumeweza kufahamu taarifa zake na hata rangi yake!

Sayari zilizo nje ya mfumo wa Jua ni ndogo sana na vigumu sana kuweza kuziona. Ni kama haiwezekani kabisa kufahamu taarifa zake.

Kwa bahati nzuri, wanaastronomia wana njia za kuweza kuzichunguza.

Sayari zilizo nje ya mfumo wa Jua hazitengenezi mwanga wake zenyewe, lakini zina uwezo wa kuakisi mwanga wa nyota zinazo zizunguka. Kwa kupima kiasi cha mwanga kinachoakisiwa na sayari hizo, tunaweza kuchakata taarifa mbali mbali zinazozihusu ikiwemo rangi.

Nyuso kama za theluji na barafu zinaakisi mwanga mwingi, na nyuso nyeusi kama za majani na lami zinaakisi mwanga kidogo.

Sayari mpya iliyogunduliwa ni nyeusi sana kama lami mbichi na inafyonza kiasi kikubwa cha mwanga wa nyota unaotua katika uso wake. Ni kiasi cha asilimia 10 tu cha mwanga unaotua unaakisiwa. Ili kuweza kuelewa, Mwezi unaozunguka Dunia unaakisi mara mbili ya mwanga wake.

Rangi yake inaendana na jotoridi katika sayari hiyo, linalofikia zaidi ya nyuzi joto 2,000. Joto hili la juu sana linaathiri angahewa la sayari hii na kuzuia mawingu kutengenezwa, ambayo yangeweza kuakisi mwanga zaidi.

Dokezo

Kitu chenye kuakisi mwanga zaidi katika mfumo wetu wa Jua ni mwezi wa sayari ya SATANI ambao umefunikwa na barafu, uitwao Enceladus (“en-SELL –ah-dus”). Mwezi unaozunguka sayari yetu ya Dunia­ huakisi asilimia kumi na nne (14%) ya mwanga wa Jua unaotua juu yake, wakati Enceladus huakisi zaidi ya asilimia tisini na tisa (99%) ya mwanga utuao!

This Space Scoop is based on a Press Release from Hubble Space Telescope .
Hubble Space Telescope

Gidion Kaweah / UNAWE Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi