Ukungu wa Ulimwengu Hapo Mwanzo
Okt. 12, 2011
Je ulishawahi kuamka asubuhi na kuona ukungu mzito nje, halafu ghafla jua linachomoza na kuufanya ukungu huo utoweke? Kitu kama hiko kilishawahi kuutokea ulimwengu ulipokuwa bado mdogo.
Wakati nyota za kwanza na galaxi zilipotengenezwa, ulimwengu ulikuwa umetandwa na ukungu mzito wa gesi ya haidrojeni, ambao ulifanya miale ya mwanga wa nyota isiweze kusafiri angani. Picha iliyopo hapo juu ambayo umechorwa kwa kutumia computer inaonyesha jinsi galaxi hizo zilivyokuwa zikionekana.
Nyota za mwanzo kabisa katika ulimwenguni zilikuwa kubwa sana. “Karibu mara 100 zaidi ya ukubwa wa Jua” anasema mwanaastronomia Eros Vanzella. Nyota hizi zilitoa mwanga mkali sana wa UV. (Tunaufahamu mwanga wa UV kama mionzi ya jua inayoharibu ngozi). Mwanga huu wa UV mara ukafanya ukungu uliokuwepo upotee na kufanya miale ya mwanga ya nyota iweze kusafiri angani bila kikwazo.
Katika siku za hivi karibuni wanaastronomia wametumia telescope iitwayo Very Large Telescope, ambayo ipo Chile katika bara la Amerika ya Kusini, kuangalia nyakati zilizopita na kuchunguza baadhi ya galaxi katika wakati ambapo ukungu ulianza kutoweka. (Ili kufahamu wanaastronomia wanawezaje kuangalia galaxi katika wakati uliopita bofya hapa).
Wanaastronomia waligundua kuna kitu cha kushangaza: Katika mda mfupi uliopo kati ya nyota za zamani na zile zilizo changa katika project yao ya kuangalia nyota zilizozaliwa, ambapo ulimwengu ulitoka kuwa na ukungu hadi kuwa na anga wazi. Kitu ambacho kilitokea haraka mno tofauti na walivyokuwa wakifikiri wanaastronomia hapo mwanzo, anasema mwanaastronomia Laura Pentericci.
Dokezo
Ingawa galaxi walizoziangalia ni baadhi ya galaxi zilizotengenezwa mwanzo kabisa, zilizaliwa wakati ulimwengu ulipokuwa na umri wa miaka kati ya million 780 na 980! Lakini kwa vile dunia ina umri wa miaka bilioni 13.7, bado tunachukulia wakati huo kuwa ulikuwa mdogo mno kwani bado haukufikia hata birthday yake ya miaka bilioni 1!
This Space Scoop is based on a Press Release from
ESO
.
Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania
Picha
Chapisha
Bado una shauku? Jifunze zaidi...
Space Scoop ni nini?
Vumbua astronomia zaidi
Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga
Marafiki wa Space Scoop