Kuangalia Vitu Katika Mwanga Tofauti
Mei 31, 2012

Pindi Jua linapoanza kuangaza mara baada ya mvua kunyesha, unaweza ukaona upinde mzuri wa mvua angani. Hii ni kwa sababu matone ya mvua huwa yanabaki angani mara baada ya mvua kukatika na kusababisha mwanga wa Jua kutawanywa katika rangi zote za upinde wa mvua. Na sasa siri ya rangi za upinde wa mvua imefichuliwa.

Lakini mwanga una siri nyingi zaidi. Kwa mfano, Je ulijua kuwa mwanga tunaoweza kuuangalia na macho yetu ni aina moja tu ya aina nyingi za mianga? Labda unaweza kuwa unazifahamu aina nyingine, lakini ulikuwa hutambui kuwa ni aina za mianga, kwa mfano mawimbi ya redio na miale ya microwave. Hii ni kwa sababu watu wakiwa wanazungumza kuhusiana na aina tunazoweza kuziona kwa macho yetu, huwa wanatumia jina la mwanga badala ya kusema mwanga uonekanao “visible light”.

Wakati macho yetu yana uwezo wa kuona mwanga uonekanao tu, kamera maalum zinaweza kutambua aina nyingine za mwanga. Vitu huonekana tofauti kabisa ukivipiga picha katika aina tofauti tofauti za mwanga. Kwa mfano picha hii mpya ya galaxi iitwayo Centaurus A iliyotengenezwa kwa kuunganisha picha za galaxi zilizochukuliwa kwa kutumia telescope inayoweza kutambua mianga ya redio na infrared. Na sasa angalia na fananisha na picha ya Swahili space scoop ya wiki mbili zilizopita ya galaxi hiyo hiyo ambayo iliyopigwa picha katika mwanga uonekanao.

Picha zote zinaonyesha galaxi hiyo hiyo, lakini zinaonekana tofauti kabisa, na picha inayoonyesha galaxi katika mwanga uonekanao ni nzuri zaidi. Lakini picha zote mbili zinatoa taarifa muhimu mbali mbali kwa wanaastronomia. Hivyo kutokana na kuchunguza vitu katika aina mbali mbali za mianga wanaastronomia wanaweza kuelewa ni nini kinaendelea katika ulimwengu.

Dokezo

Ni kwa kiasi cha 4% ya vitu vyote vilivyopo ulimwenguni ndio vyenye uwezo wa kutoa mwanga wa aina yeyote.

This Space Scoop is based on a Press Release from ESO .
ESO

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi