Regista ya Ulimwengu
Juni 20, 2012

Picha hii mpya inaonyesha mchirizi wa vumbi ukikatiza katikati ya wingu lililoko angani lililojaa vumbi na gesi liitwalo “NGC 6357”. (Mmmh Jina gani hili!) Ikionyesha sehemu ndogo tu ya NGC 6357 kama inavyoonekana katika picha, kitu ambacho kinaifanya picha hii iwe maalum. Picha hii imebeba taarifa nyingi sana kuliko picha nyingine zilizowahi kuchukuliwa katika eneo hili la anga.

Jina “NGC” linasimama badala ya “New General Catalogue” ambacho ni kama kitabu cha taarifa cha ulimwengu (regista), chenye orodha  ndefu sana ya vitu vilivyopo mbali kabisa angani kinachomilikiwa na wanasayansi ya astronomia. Hii ni kwa sababu kinajumuisha aina zote za vitu vilivyopo mbali kabisa angani kama galaxi na nebula (“nebula” ni jina la kitaalamu la mawingu ya gesi na vumbi yapatikanayo angani, kama hili lililoonyeshwa kwenye picha). Regista nyingine zilizopo sasa zinaorodhesha baadhi tu ya vitu maalum na muhimu.

Dokezo

Regista hii mpya ina orodha ya vitu zaidi ya 7,840!

This Space Scoop is based on a Press Release from ESO .
ESO

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi