Je ulikuwa unafahamu kuwa sukari ina vimelea muhimu vya uhai? Ingawa hii haimaanishi kuwa kula vitu vitamu kwa wingi ni kuongeza uhai. Sukari imetengenezwa kwa fomula rahisi iliyotokana na kemikali ziitwazo carbon, hydrogen na oxygen. Kemikali hizi ndizo zilizojenga karibu kila mwili wa kiumbe hai anayepatika hapa duniani pamoja na kemikali nyingine ya nitrogen.
Hivyo basi timu ya wanaastronomia kwa kutumia telescope yenye nguvu wameweza kuona sukari kwenye gesi zinazopatikana kuzunguka nyota ndogo yenye ukubwa sawa na Jua letu. Sukari ilishawahi kuonekana angani, lakini hii ni mara ya kwanza kuonekana kwa ukaribu katika nyota inayofanana na Jua. (Umbali uliopo kati ya sukari hii na jua ni sawa na umbali uliopo kati ya Jua na sayari ya Uranusi). Na kwa vile sukari ina vimelea vya maisha, kuonekana kwake karibu na nyota inayofanana na jua ni habari nzuri sana. Kitu ambacho kinaonyesha kuwa maisha kama yetu yanawezekana kupatikana katika sayari nyingine ulimwenguni!
Wanaanga hawa wamegundua pia, sukari hii huingia ndani kuelekea katika nyota. “ Sukari hii siyo tu kwamba ipo katika sehemu sahihi ya kuweza kuingia kwenye sayari, lakini pia inasogea kuelekea katika uelekeo sahihi” anasema mwanaastronomia Cécile Favre.
Jihusishe: Je ni kitu gani ungeweza kukigundua kama ungekuwa unashughulika na moja kati ya telescope kubwa zaidi Duniani? Papo hapo ili kusheherekea miaka 50 ya Kituo cha Anga cha Ulaya Kusini unaombwa kupiga kura juu ya kitu umbacho ungependa kichunguzwe na telescope yake kubwa iitwayo VLT! Bofya hapa kwa taarifa zaidi
Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania