Anga Inazeeka!
Sep. 12, 2012

Kuna wakati ni vigumu kutambua mda uliopita kati ya tukio moja na lingine lililowahi kutokea ulimwenguni. Ingawa Ulimwengu ni mkubwa na umekuwepo kwa mda mrefu sana- miaka 13.7 billioni! Umri ambao ni karibu mara tatu ya umri wa Dunia, hivyo ni vigumu kuwaza juu ya kipindi kalichopita kabla ya sayari yetu kutengenezwa! 

Tofauti hii kubwa ya wakati inawafanya wanaastronomia washindwe kuchunguzia vitu kama vile maisha ya nyota kwa kuisoma nyota moja moja, kwani itaweza kuchukua mamilioni au mabilioni ya miaka! Badala yake wanachunguza nyota mbali mbali katika vipindi tofauti tofauti vya maisha. 

Kuna wakati vitu vilivyopo mbali sana huko angani hubadilika wakati wa usiku ndani ya maisha yetu. Kwa mfano ukiangalia picha hii mpya kutoka angani, inayoonyesha mawingu ya gesi yenye kuwaka ambayo ni mabaki ya mlipuko wa nyota kubwa ulitokea karibu miaka 11,000 iliyopita. Wanaastronomia huita mlipuko kama huu supanova. 

Mawingu haya yanasafiri haraka sana huko angani, katika mwendo wa 650,000 kilometa kwa saa. Cha kuustajabisha ni kwamba, ingawa yapo mbali sana kutoka Duniani mwenod wake wa haraka sana husababisha yahame kutoka sehemu moja kwenda nyingine katika anga ya usiku ndani ya umri wa maisha ya binadamu. Nyota ambazo zipo jirani na wingu hili kwa wakati wa usiku zitabadilika kwa kadri unavyokuwa mkubwa tofauti na zile zinazooneka karibu na hili wingu kwa sasa.

Na hata baada ya miaka 11,000 milipuko ya supanova bado itabadilisha uso wa anga ya usiku! 

Jihusishe: Wanaastronomia wengi huweka kumbu kumbu ya vitu wanavyovifanya. Taarifa wanazozihifadhi ni muhimu ili kufahamu kama kuna mabadiliko yeyote ulimwenguni. Je ni kwanini usianzishe tabia ya kuweka kumbu kumbu zako binafsi? Hata kama huna telescope unaweza kuchora michoro yako mwenyewe ya vitu unavyoweza kuviona kama vile Mwezi au vitu adimu kama vimondo. 

Dokezo
None
This Space Scoop is based on a Press Release from ESO .
ESO

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi