Unanizungusha
Okt. 10, 2012
Je ushawahi kuvuta uzi kutoka katika nguo yako na kuoangalia jinsi unavyojikunjua? Wanaastronomia wameweza kuona kitu kinachofanana na hicho angani! Nyota mbili zinazozungukana katika mfumo unaoitwa pacha “binary system”, ambapo nyota moja ikiwa inatembea inavuta vitu vyote vinavyoelea karibu na nyota nyezake na kutengeneza mduara wa kupendeza wa vitu hivyo katika mfano wa kisahani!
Nyota inayoonekana katika picha hii inaitwa red giant. Nyota ambayo ilikuwa na ukubwa wa kati kati (kama jua letu), lakini jinsi inavyozidi kuzeeka inazidi kutanuka na ingawa ilikua sana lakini haikuweza kutengeneza joto la ziada, hivyo ikapoa, na kwa kadri jotoridi lake lilivyozidi kupungua, nyota ndivyo ilivyozidi kuwa nyekundu. Hili linaweza kuwa ni jambo la kustaajabisha, kwani tumezoea kuona vitu vya moto vikiwa vyekundu katika maisha yetu ya kila siku kama kwenye mabomba ya maji. Lakini katika astronomia ni kinyume chake. Hivyo basi nyota zenye joto kali zina rangi ya blue na zenye joto dogo ni nyekundu!
Nyota hii ya Red Giant inaweza kukua mara kumi au mia moja zaidi ya Jua. Nyota hii inakuwa kubwa sana mpaka inapata shida kuweza kushikilia tabaka lake la nje, ambapo hufikia wakati hupoteza kiasi kukubwa cha maada zilizopo katika tabaka lake la nje katika anga la mbali. Mwisho kabisa nyota hiyo huishia kuzingirwa na gamba kubwa la gesi na vumbi. Pia ni karibu kila nyota huishia katika hatua hii ya reg giant na kufunikwa katika wingu la gesi na vumbi za angani.
Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa wanaastronomia kuona gesi zinazowaka zikizunguka katika mduara huko angani! Mfumo huu wa kushangaza unaweza kutengenezwa na nyota pacha isiyoonekana tu. Nyota ambayo ni hafifu sana kwa sisi kuiona, ingawa imejidhihirisha kwa kupitia mduara huu wa angani!
Dokezo
Reg Giant hurusha maada nyingi sana angani na kutoa mchango mkubwa sana katika gesi na vumbi linalopatikana angani kwa ajili ya kutengeneza nyota mpya na sayari, na pia huchangia katika uwepo kwa maisha. Ambapo upo uwezekano kuwa na wewe una red giant katika mwili wako!
This Space Scoop is based on Press Releases from
SAAO
,
ESO
.
Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania
Picha
Chapisha
Bado una shauku? Jifunze zaidi...
Space Scoop ni nini?
Vumbua astronomia zaidi
Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga
Marafiki wa Space Scoop