Kutoka Mtu Mdogo wa Kijani hadi Galaxi Kubwa ya Kijani!
Dis. 5, 2012
Kuna watu bilioni saba wengine wanaoishi katika sayari hii pamoja na wewe, watu wenye umri, ukubwa na rangi za ngozi tofauti tofauti. Ingawa kuna karibu ya mara mamilioni ya galaxy katika ulimwengu zaidi ya binadamu! Nazo pia zipo katika namna tofauti tofauti.
Hivi karibuni aina mpya ya galaxi imeongezwa katika orodha. Aina hii mpya ni kubwa na inang’aa kuliko kitu kingine chochote angani, na kama hiyo haitoshi, basi pia zinawaka katika mwanga wa kijani! Hii imewafanya wanaastronomia wazipe jina la ‘green bean’(harage la kijani) galaxy (angalia green bean ndogo ndogo katika picha iliyopigwa angani).
Galaxi hizi mpya ni baadhi ya vitu adimu sana katika ulimwengu kwa ujumla. Tunafikiri kuwa zinang’aa sana kwa sababu ya shimo jeusi katika viini vyake. Shimo jeusi ni kitu kidogo sana ambacho kina nguvu kubwa ya uvutano. Ambapo kitu chochote kinachosogea karibu na shimo jeusi kinavutwa ndani ya shimo hilo na kutokuonekana tena. Karibu kila galaxy ina kitu kama hicho cha ajabu katika kiini chake, ikiwemo galaxi yetu ya Milk Way!
Kama vile shimo jeusi linavyomeza vitu vilivyo karibu yake na vile vinavyolizunguka. Fikiria kama vile maji yanavyofonzwa katika sinki. Mduara unaozunguka shimo jeusi huongezeka joto kwa kadri jinsi unavyozungushwa na kufanya utoe mwanga mkubwa sana unaong’aa. Kwa kutumia njia hiyo mashimo meusi yanajulikana kwa kutengeneza mwanga mkali kabisa katika viini vya galaxy. Lakini katika green beans, galaxi yote inawaka!
Dokezo
Pamoja na green beans (maharage ya kijani), kuna galaxi za ‘green pea’ (njegere) pia huko angani. Zilizopewa jina hilo kwa sababu zinafanana na njegere (angalia hapa). Galaxi hizi ni ndogo kuliko zile za green bean na zinatoa mwanga mkali sana wa kijani unaotoka kwenye nyota zilizopo ndani yake!
This Space Scoop is based on a Press Release from
ESO
.
Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania
Picha
Chapisha
Bado una shauku? Jifunze zaidi...
Space Scoop ni nini?
Vumbua astronomia zaidi
Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga
Marafiki wa Space Scoop