Mfyonza Gesi Mkubwa
Jan. 2, 2013

Unajua kuwa umetengenezwa kwa vumbi la nyota? Ni kweli, sote tumetengenezwa kwa vumbi la nyota na pia Dunia yetu! Karibu kila kitu kimetengenezwa na maada ambazo zimetengenezwa kutoka katikati ya nyota. Kitu chochote ambacho hakikutengenezwa katika nyota, kimetengenezwa na maada sawa sawa na zile za nyota — sayari za gesi mfano Jupita na Satani. Mara baada ya kujua kuwa sayari zimetengenezwa kwa mabaki yaliyotokana na kutengeneza nyota, sasa kifuatacho kinaleta maana! 

Nyota inapozaliwa, ndani kabisa ya wingu la gesi na vumbi la angani, mabaki yote yaliyobakia hutengeneza visahani (kama pete za Satani) kuizunguka. Vipande vidogo vya miamba ndani ya visahani hivyo hugongana ambapo kuna wakati hushikamana na kutengeneza kitu kikubwa na kikubwa zaidi. Ambavyo ndivyo sayari zinavyozaliwa. 

Maada zaidi zinapovutwa ndani ya sayari, hufanya sayari ikue zaidi.  Lakini sayari zinakula vibaya sana. Huwa zinafyonza gesi kutoka katika visahani na kutengeneza katika mkondo mrefu wa gesi. Ni vigumu sana kuona sayari yenyewe wakati inatengenezwa, kwa sababu gesi na vumbi ndani ya visahani huzificha zisionekane. Lakini kwa kutumia telescope kubwa na yenye nguvu iitwayo ALMA, wanaastronomia wamegundua mikondo hii ya gesi inayotiririka kutoka kwenye visahani vya nyota ndogo za jirani kutengeneza sayari! Kutokana na kuwa na mikondo zaidi ya mmoja, inadhaniwa kuwa kuna sayari zaidi ya moja zinazotengenezwa. 

Dokezo

Ulijua kuwa mfumo wetu wa Jua una sayari kubwa nne za gesi? Zote zipo katika sehemu ya nje ya mfumo wa Jua, baada ya Mars. Nazo ni Jupita, Satani, Uranusi na Neptuni. Jupita ni kubwa zaidi na Dunia inaweza kujazwa ndani ya Jupita mara 1,300!

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi