Kukusanya mwanga usioonekana (mwanga ambao macho yetu hayawezi kuuona) ni jambo gumu sana. Kama telescope yako ipo ardhini, basi taarifa kutoka angani zitajichanganya na taarifa kutoka katika tabaka letu la hewa. Ili kuzuia, wanaastronomia wametuma maputo juu angani yakiwa na vifaa ndani yake ili kulisoma anga. Moja kati ya maputo haya yamefika umbali wa Kilometa 50 juu!