Nzuri Ingawa ni Kifo
Jan. 28, 2013

Kuna msemo usemao “kizuri hakikosi kasoro”. Kwa mfano mnyama, mdudu au ua vikiwa na rangi rangi nyingi za kupendeza, mara nyingi pia huwa na sumu. Basi hali pia ni vivyo hivyo huko angani. Pichani ni puto la rangi ya pinki ling’aalo pembezoni mwa anga lenye nyota. Mawingu haya ya kupendeza ni ya hatari mno ingawa yanapendeza kwa macho kutokana na kutoa miale mikali mno inayoweza kusababisha kifo!

Wingu la gesi linalowaka katika picha linaitwa ‘Superbubble’ na hupatikana katika maeneo ambapo nyota nyingi na kubwa zimetengenezwa katika siku za karibuni. Nyota hizi changa hutoa upepo mkali na kufanya nyota kubwa zikue haraka haraka na kufa wakati bado ni changa. Hukua haraka haraka na kisha kulipuka katika mlipuko wa supernova. Ni nguvu hizi za usambaratisho zilizorundikana katika kiini cha wingu na kutengeneza ukingo wa gesi na vumbi.

Vurugu zinazotokea ndani ya super bubble huendelea hadi nje ya eneo la wingu katika mfumo wa mionzi hatari ya X-ray. Wanasayansi wamegundua kuwa wingu hili linatoa mionzi hiyo mara 20 zaidi ya walivyodhania! Hivyo basi kuwa mfano wa vitu vyenye kupendeza lakini vinavyoweza kusababisha kifo! Ushauri wangu ni kwamba: furahia vitu vizuri huku ukiwa katika umbali salama!

Dokezo

Supperbubble hii inapatikana ndani ya galaxi ndogo iitwayo Large Magellanic Cloud. Ndio, umekisia sawa; galaxi ndogo ni zile zenye nyota chache na ndogo kabisa ijulikanayo ina udogo mara milioni 20 ulinganisha na ya kwetu, Milk Way!

This Space Scoop is based on a Press Release from Chandra X-ray Observatory .
Chandra X-ray Observatory

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi