Ufuatiliaji Chanzo cha Miale Angani
Feb. 14, 2013

Mionzi ya angani ni chembe chembe ndogo zenye nishati kubwa, ambazo hupatikana mbali kabisa katika mfumo wetu wa Jua, ambayo hutupatia sampuli ya vitu muhimu sana kutoka katika anga za mbali. Lakini wigo wa usumaku katika galaxy na mfumo wetu wa jua hukinzana sana na miale hii na kutufanya tushindwe kufuatilia vyanzo vyake. Lakini kutokana na mabaki ya nyota iliyokufa maelfu ya miaka iliyopita, wanaastronomia wamepata fununu ya chanzo cha miale ya angani.

Katika miaka mingi iliyopita ndani ya mwaka wa 1006, nuru mpya ya mwanga ilionekana katika anga ya kusini. Ilikuwa inang’aa mno hata kupita mng’ao wa Mwezi na pia iliweza kuonekana hata wakati wa mchana! Chanzo cha kitu hiki cha ajabu ni nyota kubwa iliyokuwa ikikaribia mwisho wa maisha yake: ilikuwa inalipuka! Wanaastronomia wanauita mlipuko wa nyota ‘supernova’. Kwenda mbele miaka 1000 wanaastronomia wameweza kuonyesha michirizi ya mabaki ya nyota hiyo ya kale. Ikiwa na maada zinazowaka na nyingine katika gimba lake. Hivyo ndivyo  vilivyobakia. Unaweza kuona sehemu zima ya gimba hilo katika picha ya pili

Kwa kuangalia mabaki haya ya nyota hii iliyokufa wanaastronomia wamegundua kuwa wanaweza kugundua kitu wakiitacho chanzo cha miale ya angani. Chembe chembe hizo zinaweza kuonekana kwa kuvuta kwa ukaribu mabaki haya ya nyota. Ingawa bado hakuna nishati ya kutosha ili kutengeneza miale ya angani, wanaastronomia wanaamini  kuwa chembe chembe zilizomo zinaweza kuwa miale na kutoa mwanga kwa kugongana na maada zilizopo katika gimba hilo. Kwa njia hii chembe chembe zinaweza kupata nishati ya kutosha na kuruka kama miale!

Dokezo

Wanaastronomia wamekwishaona sehemu nzuri za kustaajabisha: Mwanga wa kaskazini katika ukingo wa Dunia na upande wa giza wa Mwezi. Zaidi ya hapo wanaastronomia waliopo kwenye chombo cha Skylab, the Shuttle, Mir na International Space Station wametoa ripoti ya kuona mianga ya angabu ing’aayo angani. Hii inasababishwa na miale ya angani inayogonga macho yako kama risasi ndogo ngogo. Kama moja ya chembe hizi zikigonga mishipa ya fahamu kwenye jicho huchochea taarifa za uongo katika ubongo zinazotafsiriwa kama mwanga unaong’aa.

This Space Scoop is based on a Press Release from ESO .
ESO

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi