Galaxi Yenye Nguvu Yaonyesha Upande Uliojificha
Feb. 20, 2013

Hii inaonekana kama picha ya sayari yenye nguvu, inayoangamiza miale kama ilivyo katika filamu ya Star Wars au filamu nyingine za kisayansi! Kitu ambacho kinaweza kuwa kweli. Tunachokiangalia hapo ni kiini kimojawapo cha galaxi yenye nguvu na kubwa katika Ulimwengu. Kiini cha galaxi kama hiki hutoa kiasi kikubwa cha nishati, inayong’aa zaidi ya mwanga wa galaxi 100 zikiletwa pamoja! 

Ingawa picha hii ni kazi ya sanaa na sio picha halisi, inatokana na picha halisi ya pande tatu (3D) ya kwanza kupigwa kwa quasar – hivi ndivyo wanaastronomia wanavyoviita viini hai vya galaxi! Kuweza kufanikiwa kuona kitu cha kiastronomia katika 3D sio kitu rahisi, labda kama kitu hiko kinazunguka, na pia ni vigumu zaidi kuona katika pande tofauti tofauti. Lakini shujaa wa kipekee alikuja kusaidia katika kazi hii: gimba kubwa la galaxi lililopo kati ya Dunia na quasar. 

Inaonekana kukanganya, ila badala ya gimba hili kuikinga quasar, nguvu ya uvutano ya galaxy ilikuwa kubwa mno na kusababisha mwanga unaotoka kwenye quasar kupinda ulipopita juu yake. Kutokana na tukio hili mwanga uliweza kupita katika gimba na kutuwezesha kuiona quasar kutoka Duniani. Cha kufurahisha zaidi ni kuwa gimba hili liliupindisha mwanga na kutuwezesha kuona mwanga unaotoka katika pande tofauti tofauti za quasar kwa mara moja! Hii iliwafanya wanaastronomia waweze kuiona galaxy hii katika pande tatu (3-D) kwa mara ya kwanza! 

Dokezo

Ulimwengu umetengezwa na vitu mbali mbali vyenye maumbo mbali mbali ambayo huletwa pamoja kwa nguvu ya uvutano! Nyota huletwa pamoja katika galaxi na galaxy huletwa pamoja katika makundi ya galaxi. Galaxi yetu ya Milky Way, ni sehemu ya kundi la Virgo pamoja na galaxi nyingine zinazokaribia 2000! 

This Space Scoop is based on a Press Release from NAOJ .
NAOJ

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi