Majirani Wapya
Machi 27, 2013

Ulimwengu ni wa zamani sana, ukiwa na miaka inayokaribia bilioni 13.8 na vitu vyote vinajuana. Galaksi yetu ya Milk Way pia ni ya zamani sana na baadhi ya nyota zake zina umri wa miaka bilioni 13. Lakini bado una sehemu zenye uhai ambapo vitu vipya huundwa na vingine kuangamizwa. Katika picha hii unaweza kuona kundi la vitu vipya katika jamii ya Jua.

Lakini nyota hizi mpya zina umri gani? Inaonekana kuwa umri wake bado haujajulikana kwa uhakika, lakini wanaastronomia wanafikiri kuwa ni kati ya miaka milioni 20 na 35. Umri huo hauonekani kuwa mdogo hata kidogo, si kweli? Lakini papo hapo, Jua letu lina miaka milioni 4600 na bado hata halijafika katikati ya maisha yake. Hii inamaanisha kuwa kama unalifikiria Jua kuwa na umri wa miaka 40 ya mtu mzima basi nyota zilizopo katika picha zitakuwa na umri wa miezi mitatu!

Nyota nyingi huwa hazijiundi peke yake. huwa zinazaliwa pamoja na mamia au maelfu ya nyota nyenzake, katika kundi. Nyota katika kundi huzaliwa kutokana na malighafi zilizo sawa na katika wakati mmoja. Picha hii inaonyesha kundi la nyota lililowazi. Nyota hizi mara nyingi huishi kwa muda mfupi pamoja, kabla hazijaanza kutawanyika moja kwa moja. Lakini kuna kitu cha kipekee katika kundi hili, lina nyota moja au mbili zenye rangi nyekundu na njano ambazo zina umri mkubwa zaidi. Unaweza kuzitambua?

Dokezo

Moja kati ya kundi la muda mrefu linalojulikana ni Messier 67. Kundi hili lina umri wa miaka bilioni 3.7! Wanaastronomia wanafikiri kuwa limeishi mda wote huo kwa sababu lipo sehemu iliyojitenga ya Milk Way, hivyo hakuna kitu chochote kizito chenye nguvu za kulitawanya.

This Space Scoop is based on a Press Release from ESO .
ESO

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi