Utambulisho Uliokosewa
Machi 28, 2013

Unaona nini unapoangalia picha hii ya angani?

Kama ulijibu galaksi, au vizuri zaidi spiral galaksi basi upo sahihi! Lakini unaweza kuamini kuwa sio mara moja bali ni mara mbili galaksi hii ilikosewa kutambuliwa na wataalamu wa astronomia? Kwa mara ya kwanza ni pale ilipotazamwa na Pierre Méchain katika mwaka wa 1780, ambapo alifikiri kuwa ni nebula (gimba la vumbi na gesi linalowaka). Halafu miaka michache baadae, Charles Messier aliita ‘star cluster’ ambalo ni kundi lenye nyota maelfu au mamilioni zilizoletwa pamoja kwa nguvu ya uvutano (makundi haya yana nyota chache mno ukilinganisha na galaksi). Usijali kuhusu Charles kwani ulikosea kwa nyota chache kama billioni 100! 

Lakini kabla hatujaanza kumkosoa Pierre na Charles inatupasa tukumbuke kuwa telescopes ndio kwanza zilikuwa zimengunduliwa katika miaka hiyo ya 1700. Ukilinganisha ubora wa telescopes hizi za mwanzo na telescope ya Hubble ya angani, ni sawa na kulinganisha gari la toi na gari aina ya Ferrari. Je unaweza kuamini kuwa tuna miaka isiyopungua 100 tangu tugundue kuwa kuna galaksi nyingine zaidi ya yetu katika ulimwengu? Ambapo siku hizi tunajua kuwa ulimwengu una mabilioni ya galaksi zilizojaa nyota. 

Galaksi hizi huja katika maumbo na ukubwa wa aina tofauti tofauti. Picha hii haionyeshi spiral galaksi peke yake, lakini pia ni mfano wa karibu wa galaksi ya ‘Seyfert’. Hii ni aina ya galaksi yenye nguvu sana, ina magimba yenye joto kali na gesi zenye kuwaka sana na pia hutoa miale mikali kutoka katika kiini chake chenye giza.

Dokezo

Katika picha moja iliyopigwa ndani ya sehemu ndogo ya anga la usiku, Hubble iliweza kupiga  picha galaksi maelfu! Unaweza kuiona picha hiyo hapa. Je imekufanya uweze kutambua ni kwa kiasi gani ulimwengu ulivyo mkubwa? 

This Space Scoop is based on Press Releases from Hubble Space Telescope , ESA .
Hubble Space Telescope ESA

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi