Yote Ya Mars Express
Juni 7, 2013

Miaka kumi iliyopita chombo cha Mars Express kiliondoka nje ya tabaka la hewa ya Duniani na kuanza safari yake kuelekea Sayari Nyekundu. Tangu wakati huo chombo hiki kimekuwa kikifanya kazi ya kutupa mwanga juu ya vitu vingi vilivyopo katika sayari hiyo. Katika muongo uliopita kimetuma picha za kustaajabisha za volkano kubwa, makorongo makubwa na vizio vyenye barafu kama vya hapa Duniani. 

Imetuonyesha bila ya shaka kuwa miaka bilioni iliyopita, sayari hii ya nne kutoka kwenye Jua ilikuwa na joto na maji mengi kuliko ilivyo leo. Ikiambatana na ramani zilizojaa taarifa na picha zenye kuonyesha jinsi mito ya zamani ilivyokuwa na sehemu za mabondeni, na hata imeweza kugundua aina za kipekee za miamba ambazo zinaweza kuwepo kwenye maji tu! Tunaishukuru mission hii, kwani imeweka dhahiri kwamba Mars hapo mwanzo iliweza kutoa mazingira mazuri kwa uwezekano wa maisha kuwepo. 

Chombo hiki hakikugundua tu kuwa maji yalikuwepo katika miaka mingi iliyopita, iliona pia maji yaliyoganda ambayo yanapatikana hata leo! Tabaka jembamba la maji yaliyoganda yapo chini ya uso wa sayari na kutapakaa katika mamia ya kilometa kuzunguka Kizio cha Kusini. Na sio katika kizio cha barafu peke yake, maji pia yanapatikana katika maziwa yaliyoganda chini ya sayari hii kavu, yenye uso wenye vumbi. Katika vizio, chombo hiki kiliona kiasi kikubwa cha maji yaliyoganda, ambapo yakiyeyuka yanaweza kufunika sayari nzima na kuwa bahari yenye kina cha mita 11! 

Mwisho kabisa inatupa tumaini kubwa kuwa sayari hii inaweza kustahimili maisha, kwani Mars Express iligundua kemikali inayoitwa “methane” katika tabaka la hewa la Mars. Katika Dunia, methane inatengenezwa na milipuko ya volkano tu au viumbe hai. Je inamaanisha kuwa kuna viumbe hai katika Mars? 

Shani hii haijaishia hapo kwani Mars Express bado ina miaka mingi ya kuishi huko! Na katika wiki hii imetuma taarifa kuhusu Mafuriko makubwa ambayo yalifunika mito na deltas katika eneo la kilometa laki tano la sayari hiyo, katika miaka bilioni tatu iliyopita! Hayo ni mafuriko ambayo yanaweza kuifunika nchi yote ya Mexico!

Dokezo

Ulijua kuwa Mars ina miezi miwili? Inaitwa ‘Phobos’ na ‘Deimos’. Chombo hiki cha Mars express kimechukua picha za kupendeza za Phobos wakati wa mission hii: ziangalie mwenyewe katika picha hii

 

This Space Scoop is based on a Press Release from ESA .
ESA

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi