MKIA WA KIMONDO KINACHOPOTEA
Ago. 31, 2017
Mara nyingi, katika mwaka, anga la usiku humulikwa kwa mamia ya vimondo vinavyowaka. Unaweza kuvifahamu hivi kama “nyota zinazotembea”, ingawa havina uhusiano wowote na nyota. Kwani ni vipande vidogo vidogo vya miamba viunguavyo katika angahewa , ambavyo tunaviita “Vimondo”.
Kuna wakati, Vimondo humurika Dunia katika makundi makubwa kama matone ya mvua. Hii huitwa “Mvua ya Vimondo”
Mvua za vimondo husababishwa na vimondo vidogo vidogo (comets). Vimondo vimetengenezwa na vumbi la angani, miamba na barafu. Vinaposafiri karibu na Jua joto la Jua hupelekea barafu kuyeyuka. Hivyo vipande vidogo vya miamba na vumbi huchomoka na kutengeneza mikia mizuri yenye kuwaka.
Wakati Dunia ikiwa inasafiri kukatiza mikia ya vimondo hivi, vipande vyake huungua katika angahewa la Dunia na kutengeneza mvua ya Vimondo.
Moja kati ya mvua za kupendeza za vimondo ni “Phoenicids” (inatamkwa “FEE-ni-kids”). Phoenicids iliangaza anga letu mwaka 1956…..na haijawahi kujirudia tena. Wanaastronomia waliachwa na bumbuwazi: ni wapi mvua ya Phoenicids ilitokea na ni wapi ilitokomea?
Katika kutafuta jibu la swali hili, walienda kutafuta kimondo kilichopotea kiitwacho Blanpain.
Mwaka 1819, wanaastronomia wawili walikigundua Kimondo Blanpain. Lakini mwisho wa mwaka kilipotea kimaajabu.
Baada ya miaka takribani 200 kupita, kimondo kikubwa kilionekana kikisafiri katika njia sawa na ile ya kimondo Blanpain.
Mabarafu, gesi na mavumbi yote ambayo huenda yaliponyoka kutoka kwenye kimondo, bado yanaelea ulimwenguni kama mchirizi mwembamba wa vumbi unaoelea. Pia kama kimondo kikubwa yanafuata njia ileile iliyopitiwa na kimondo cha Blanpain.
Pindi mchirizi huu wa vumbi la kimondo Blanpain unapogongana na Dunia, vipande vyake huliangaza anga kama mvua ya vimondo (Phoenicid)!