Kuzunguka wa Shimo Jeusi Huongeza Mawimbi ya Radio
Jan. 14, 2018

WanaAstronomia wamegundua njia mpya ya kuongeza Radio: usijali kuhusu kuzungusha kitufe cha sauti, jaribu kulizungusha shimo kubwa jeusi!

 

Nyimbo tunazozisikia zikiimbwa Redioni ni mawimbi ya sauti ambayo husafiri kutoka kwenye Redio hadi kwenye masikio yetu. Mawimbi haya hutumwa kwenye Redio na“Mawimbi yaitwayo Radio”. Mawimbi ya Radio ni aina ya mwanga ambao hauwezi kuonekana kwa macho, na pia siyo aina ya sauti.

 

Mawimbi ya Radio hutuma muziki, picha na data kwa namna isiyoonekana hewani. Hili hufanyika katika mazingira yanayotuzunguka wakati wote, katika maelfu ya njia tofauti. Simu za mikononi, Wi-Fi na maelfu ya teknolojia za mawasiliano ya bila nyaya, zote hutumia mawimbi ya Radio kuwasiliana.

 

Mawimbia ya Radio pia huifikia Dunia kutoka Anga za mbali. Sayari, Nyota na makundi nyota vyote huzalisha mawimbi ya Radio. Lakini chanzo kikubwa cha mawimbi haya ni mashimo meusi makubwa.

 

Katika mchoro wa sanaa hapo juu, shimo kubwa jeusi linameza vitu. Kabla ya vitu hivi kupotea daima, maada za nyota huzungushwa kwa mwendokasi mkubwa sana kulizunguka shimo jeusi. Maada hizi zinazosafiri kwa mwendokasi mkubwa hufyatua mionzi mikubwa ya mawimbi ya Radio angani.

 

Lakini siyo mashimo meusi yote huzalisha kiasi sawa cha mawimbi ya Radio. Jambo hili kwa muda mwingi limekuwa likiwaduwaza wanaAstronomia.

 

Hivi karibuni, timu ya Wanasyansi waliamua kuchunguza kwa ukaribu kwanini hili linatokea. Walichunguza kwa umakini mashimo meusi makubwa 8,000, ambayo baadhi yalitoa miali ya Radio mikali na mengine hayakutoa. Kupitia uchunguzi wao, inaonekana wanaweza kuwa jawabu limeptakana: Kasi ya Kuzunguka

 

Ulimwengu umejaa vitu vinavyozunguka: Dunia, Jua na makundi ya nyota, bila kusahau mashimo meusi. Kulingana na matokeo haya mapya, inaonekana kuwa mashimo meusi yanayozunguka kwa mwendokasi mkubwa zaidi ndiyo hutoa miali mikali ya mawimbi ya Radio.

Dokezo

Labda kitokee kitu cha kuyazuia, lakini mawimbi ya Radio yanaweza kusafiri milele. Kuna uwezekano wa kuwepo mawimbi ya Radio ambayo yamesafiri hadi nje ya mfumo wetu wa Jua. Je, ni nini jamii za viumbe wageni (Alien) wataweza kufikiri watakapousikia wimbo wa Beyonce?

This Space Scoop is based on a Press Release from NAOJ .
NAOJ

Kaweah, Gidion Anderson / UNAWE TANZANIA

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi