Katika Tufani ya Vimondo
Jan. 21, 2018

Je, unaishi katika sehemu Duniani ambayo huwa inakumbwa na tufani ya vumbi au theluji? Kwa wengi wetu mabadiliko makubwa ya hali ya hewa kama tufani iliyoambatana na mvua au upepo, huleta madhara makubwa katika maisha yetu ya kila siku. Theluji na upepo huweza kuzuia usafiri na kukatika kwa nishati ya umeme, hali joto na mawasiliano, na mwingine hali hii inaweza kuwa kwa siku kadhaa mfululizo.

 

Kati ya mwaka 2014 na 2016 kifaa cha angani kilichojulikana kwa jina la Rosetta kilipaa kando kando ya kimondo 69 P (Comet 67P). Katika kipindi hiki cha miaka miwili, Rosetta ilikumbana na janga kubwa la kuchafuka kwa hali ya hewa kama tunavyoweza kupata hapa Duniani.

 

Picha hii ilipigwa na Rosetta wakati ilipokuwa ikipaa pembezoni mwa kimondo 69P. Japokuwa inawezakuonekana kama tufani ya theluji, vinayoonekana ni vipande vya vumbi mbele ya kamera ya Rosetta. Vimondo mara nyingine hujulikana kama “Matufe machafu ya theluji” kwa sababu vimetengenezwa kwa theluji na mavumbi. Vimondo vinaposafiri na kufika karibu na Jua, joto la Jua huvipasha joto na kusababisha theluji kuyeyuka na mvuke wake kupotelea angani, huku ukiwa unabeba vumbi. Wakati Rosetta ilipokuwa ikisafiri karibu na kimondo 69P, ilikumbana na tufani za namna hii nyingi na kugongwa na chenga za mavumbi.

 

Lakini licha ya hatari zake zote , vumbi hili lina matokeo ya kuvutia kwa Wanasayansi Duniani. Wakati wa maisha yake, Rosetta ilichunguza makumi ya maelfu ya chenga za vumbi, na kutoa taarifa ambazo zinawasiadia wanasayansi kutambua vitu vya msingi vinavyoutengeneza mfumo wetu wa Jua.

Dokezo

Kama ilivyo kwa vifaa vingi vya angani, Rosetta ilitumia nyota katika kusafiri angani. Hata hivyo, mara kwa mara vifaa vyake vya kuzitambua nyota vilikuwa vinazubaishwa kwa chenga za mavumbi vikidhani kuwa ni nyota wakati wa kusafiri!

This Space Scoop is based on a Press Release from ESA .
ESA

Kaweah, Gidion Anderson / UNAWE TANZANIA

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi