Tafadhali Usizime Mziki!
Ago. 15, 2012
Je ulikuwa unajua kuwa sauti tunazozisikia hapa Duniani ni mitikisiko ya hewa? Ingawa hii haimaanishi kwaba huko angani juu ambapo pametulia kuwa hakuna hewa yeyote. Hii ni kwa sababu hewa ni mkusanyiko wa gesi na huko angani kumejaa mawingu ya gesi ambayo yanaweza kutikisika na kufanya sauti iweze kusafiri angani.
Kutokana na hivyo tunaweza kujua ni jinsi gani sauti inavyoweza kusafiri angani, lakini je ni nini kinachofanya makelele tunayoyasikia angani? Jibu ni kwamba kuna vitu vikubwa sana vyenye uwezo wa kutoa nguvu kubwa au nishati yenye uwezo wa kufanya gesi za angani zitikisike.
Kwa mfano, shimo jeusi zaidi ya kuwa na uwezo wa kumeza vitu pia lina uwezo wa kutoa milipuko yenye nguvu/nishati nyingi. Tayari wanaastronomia wanafahamu kuwa shimo jeusi lililopo kati kati ya mkusanyiko wa galaxi uitwao Perseus Cluster (Mkusanyiko wa Perseus) lina nguvu ya kutosha kuweza kutengeneza sauti nzito angani.
“Mwanzoni tulikuwa tunafikiria kuwa sauti hizi nzito zinaweza kusikika katika mikusanyiko yote ya galaxi ulimwenguni” anasema mwanaastronomia Ryan Foley. Ryan ni mjumbe wa timu ya wanaastronomia ambao katika kipindi cha karibuni waliweza kuchunguza mkusanyiko wa Phoenix (Phoenix Cluster) angalia picha hapo juu. Mkusanyiko huu kwa ujumla upo kimya sana na hii inamaanisha kuwa si mikusanyiko yote ya galaxi yenye uwezo wa kutengeneza sauti na kama si hivyo basi kuna wakati mziki kutoka kwenye mikusanyiko ya galaxi huzimika!
Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania
Picha
Chapisha
Bado una shauku? Jifunze zaidi...
Space Scoop ni nini?
Vumbua astronomia zaidi
Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga
Marafiki wa Space Scoop