Mgongano wa Galaxi
Dis. 6, 2012

Ulimwengu ni mkubwa mno na umetengenezwa na sehemu zilizo wazi, lakini kugongana kwa vitu vilivyomo humo bado ni suala linalotokea mara kwa mara. Galaxi iliyoonyeshwa katika picha pii, inaonekana kama ubao mkubwa wa kulenga shabaha, na katika miaka 300 ya mwanga iliyopita, galaxi nyingine ndogo iliweza kujigonga katikati ya galaxi hii. 

Galaxi hii ilianza maisha yake kama galaxi mzunguko. Ilikuwa na mikono mirefu iliyopinda, iliyotokana na nyota na vumbi zilizozivilingisha katika kiini chake, kama galaxi katika picha hii. Lakini mgongano na galaxi ndogo uliathiri mpangilio wake wa nyota na pia kiini chake na kuifanya galaxi hii iwe na umbo hili lililopinda pinda. Unaweza kuona kuwa, sehemu inayong’aa ya kati yenye gesi imesogezwa kuelekea upande mmoja na mikono iliyopinda imebadilishwa katika mpangilio usio eleweka. Sehemu moja ya mkono wake iliyobaki inaonekana kuongezeka kuelekea juu, juu kabisa ya galaxi. 

Mgongano huu pia ulitengeneza mawimbi, kama yale yanayotokea ukitupa jiwe kwenye maji yaliyotulia. Gesi katika galaxy nzima ziliathiriwa na mawimbi hayo na kuanzisha mnyororo wa matukio ya nyota kuzaliwa. Mamia ya nyota mpya zenye nguvu zilizaliwa. Unaweza kuziona nyota hizo zenye kung’aa katika ukanda wa blue katika picha ya pili kulia. 

Dokezo

Milk Way pia inatarajia kupata sura mpya, miaka bilioni 4 kutoka sasa, ambapo itagongana na galaxi kubwa iliyo jirani yetu iitwayo Andromeda. Jua linaweza kutupwa katika sehemu tofauti kabisa ya galaxi. Unaweza ukatafakari kuangalia anga jipya kabisa? 

This Space Scoop is based on Press Releases from Chandra X-ray Observatory , ESA .
Chandra X-ray Observatory ESA

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi