Hongera, Kweli…ni Sayari!?
Feb. 28, 2013

Wakati mwanamke ni mjamzito,inabidi aende akapige ultrasound ili daktari aweze kuangalia ndani ya tumbo lake ili amwangalie mtoto jinsi anavyokuwa ndani. Wanaastronomia wamefanya uchunguzi kama huo katika siku za karibuni kwa nyota iloyopo jirani kabisa na sisi. Ila ni kwa bahati mbaya! wakati walipokuwa wanaangalia wingu zito la gesi linaloizunguka nyota na walishangaa kuona sayari changa inayokuwa ndani yake! Kwa mara ya kwanza sayari imeweza kuonekana katika hatua za mwanzo kabisa za kufanyika kwake. Picha hii ni kazi ya sanaa inayoonyesha jinsi sayari hiyo inavyoweza kuonekana kwa ukaribu. 

Wanaastronomia huziita sayari zilizopo nje ya mfumo wetu wa Jua ‘Exo-Planets’ sayari za nje. Utafutaji wa sayari za nje ni moja kati ya mada zenye kusisimua sana katika astronomia kwa sasa. Karibu sayari 850 zimeshagunduliwa hadi sasa, lakini kuzipiga picha kwa ukaribu kama hivi moja kwa moja bado ni mara chache sana. Hii inatokana na sababu kuwa sayari zina mwanga hafifu kuliko nyota na mara nyingi hukigwa na mwanga wa nyota. Ni sawa na kujaribu kuiona ndege ipitayo mbele ya mwanga wa Jua unaowaka sana. 

Nyota hii changa sasa inajulikana kuwa na sayari moja inayoizunguka katika umbali wa mara sita ukilinganisha na wa Dunia kutoka kwenye Jua. Sayari hii mpya ipo umbali wa mara kumi zaidi! Wakati sayari hiyo ingali bado changa sana, pia sio ndogo sana kwani wanaastronomia wanaikadiria kuwa na ukubwa kama wa Jupita, ambayo inaweza kumeza sayari kama Dunia 1000 ndani yake! 

Wanaastronomia wanafikiria kuwa sayari kubwa zinakuwa kutokana na kuchukua mabaki ya gesi na vumbi baada ya nyota kutengenezwa. Utafiti mpya unathibitisha hili: kwani sayari hii ipo ndani kabisa ya wingu kubwa la gesi na bado kuna sehemu nyingi ambapo nyota na sayari zinaingiliana moja kwa moja. 

Dokezo

Sayari kubwa ya nje iliiyowahi kugunduliwa ilipewa jina la kushangaza sana ‘CD-35 2722’. Sayari hii ina ukubwa wa mara 10,000 zaidi ya Dunian! 

This Space Scoop is based on a Press Release from ESO .
ESO

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi