Miale Yenye Utata
Mei 29, 2013

Pale nyota kubwa inapofikia mwisho wa maisha yake, huwa haizimiki kimya kimya kama mshumaa. Badala yake, huzimika kwa kishindo, au mlipuko mkubwa wenye mwanga mwingi kupita kitu kingine chochote katika Ulimwengu! Mlipuko huu unaitwa supanova, na ukitokea huicharanga nyota katika vipande vipande na kuvitupa katika anga. Lakini kuna kitu ambacho huwa kinabaki — kiini cha nyota kubwa baada ya kulipuka — nyota ya ‘neutron.

Picha hii naweza kuonekana ya ni ya ajabu ila inaonyesha kazi ya sanaa inayoashiria aina ya kipekee kabisa ya nyota ya neutron iitwayo “magnetar”.

Magnetars ni baadhi ya vitu vyenye nguvu iliyokithiri katika ulimwengu. Ni aina ya neutron ambayo ni ndogo na yenye vitu vilivyokandamizwa sana, ambayo hulipuka bila mpangilio na kutoa miale yenye nguvu mno.Nyota aina hii zilipewa jina kutokana na kuwa na nguvu kubwa ya usumaku. Nafikiri utakuwa umeshawahi kucheza na sumaku shuleni na kujua kuwa sumaku huvuta vitu kama chuma.

Magnetars zina nguvu kubwa ya usumaku – nguvu kubwa kabisa katika Ulimwengu mzima. Ijapokuwa hii iliyoonyeshwa kwenye picha “SGR 0418”haipo hivvo, ni dhaifu sana ukilinganisha na nyota nyingine za jamii yake.

Kitu kinachofanya hii iwe ya kustajabisha ni kwamba inaibua swali:Je nguvu inayoifanya itoe miale ya nguvu inatoka wapi? Mpaka sasa wanaastronomia wanafikiri kuwa nguvu ya usumaku inatokana na miale, lakini nadharia hii haifanyi kazi katika SGR 0418! Hii nyota inaonekana kuwa ya kipekee kati ya za zile za kipekee!

 

Dokezo

Je unajua? Dunia nayo ni sumaku kubwa! Ingawa nguvu yake haikaribiani hata chembe na ile ya magnetar, ila ina nguvu ya kutusha ya kutulinda sisi kutokana na mionzi hatari inayotoka kwenye Jua, na kusababisha rangi za kupendeza za Kaskazini!

 

This Space Scoop is based on a Press Release from Chandra X-ray Observatory .
Chandra X-ray Observatory

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi