Mbio za Nyota Angani
Juni 28, 2012

Hakuna kitu chochote angani ambacho kimesimama, nyota nyingi husogea kama wanariadha wa mbio ndefu ambao hawasimami hadi wafikie mstari wa mwisho, vivyo hivyo nyota huwa zimasogea huko angani ijapokuwa zenyewe hutembea maisha yao yote. Ingawa katika siku za hivi karibuni wanaastronomia wameweza kutambua nyota ambayo inafananishwa wa wakimbiaji wa mbio fupi  (angalia nyota iliyozungushiwa katika boxi kwenye picha ).

Ili kuweza kufahamu mwendo kasi wa nyota hii wanaastronomia ilibidi watambue umbali iliyotembea tangu ilipoanza kusogea na kwa mda gani ilichukua kufika umbali huo. Wanaastronomia hawa wanafikiri kuwa nyota hii imeanza safari yake kutokea kati kati ya wingu la gesi na vumbu linaloonekana kwa rangi ya zambarau katika picha. Nyota hii ni maalum kwani inazunguka kwa haraka sana na kutokana na hivyo imejumuishwa katika kundi la nyota zijulikanalo kama pulsar. Pulsar hii ilijietenga na wingu la zambarau wakati wa mlipuko uliotengeneza wingu la gesi na vumbi. 

Tathimini ya wanaastronomia imeonyesha kuwa pulsar hii inasogea katika mwendo kasi wa ajabu sana kati ya kilometa millioni 9 na 11 katika lisaa limoja! Mwendo kasi huu unaweza kuifanya nyota hii kuwa na mwendo kasi kupita pulsar zote zinazojulikana hadi leo! Ingawa bado kuna utata katika kupata cheo hicho kwani kuna pulsar nyingine ambayo imekadiliwa kuna na mwendo kasi kati ya kilometa millioni 5 na 10 lisaa limoja.

Ni jambo la kusikitisha kuwa wanaastronomia hawawezi kuzifanya nyota hizi mbili zishindane kukimbia ili kutambua ni ipi ina kasi zaidi ya mwenzake na badala yake inawabidi kukokotoa kwa umakini mahesabu yao ili kujua ipi ina mbio zaidi.

Dokezo

Kama pulsar inasogea katika mwendo kasi wa kilometa 11 kwa saa, hii inamaanisha kuwa inaweza kusafiri kuzunguka mastari wa Equator wa sayari ya Dunia katika sekunde 13!

This Space Scoop is based on a Press Release from Chandra X-ray Observatory .
Chandra X-ray Observatory

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi