Anga Inaweza Kulipuka!
Nov. 28, 2012

Mashimo meusi yana sifa mbaya kutokana na sifa yake ya kumeza kila kitu ndani yake na kuvipoteza moja kwa moja. Sifa nyingine ambayo haijulikani sana ni kwamba yana uwezo wa kutengeneza milipuko na kutupa vitu kwa nje. Wanaastronomia wameweza kugundua milipuko ya aina hii miwili ambayo yote imeweza kuvunja rekodi!

Galaxi nyingi zina mashimo meusi katika viini vyake, ikiwemo galaxi yetu ya Milk Way. Mashimo haya meusi yanaweza kuwa na uzito zaidi ya mara millioni ya ule wa Jua letu, ambao umekandamizwa katika duara dogo. Maada zilizopakiwa katika duara hilo huwa na nguvu kubwa sana ya mvutano, na kuweza kumeza hata mwanga!

Mashimo meusi yanajulikana sana kwa uwezo wake wa kuvuta maada ndani, kama vile maji yanavyoweza kumezwa katika shimo la sinki. Maada hizo hutengeneza umbo la kisahani kulizunguka shimo jeusi kwa kadri linavyozidi kumeza maada. Milipuko hii mara nyingi huonekana kutokea katika viini vya galaxi zinazowaka sana viitwavyo ‘quasars’.

Mmoja kati ya milipuko iliyogunduliwa upo mbali sana tena ni karibu kabisa katika na ukingo wa ulimwengu tunaoujua! Wakati mlipuko ule mwingine unaweza kutoka maada ambazo ni sawa na majua 400 kila mwaka! na nishati ya karibu mara 100 ya nishati ya nyota zote zinazopatikana kwenye Milk Way galaxi. Hii si nguvu ya kawaida!

Dokezo

Mashimo meusi sio mashimo kama unvyoweza kudhania na ni kinyume cha kitu kuwa kitupu. Kwani mashimo haya yamebeba maada nyingi ndani yake katika eneo dogo la anga huko ulimwenguni. Jaribu kutengeza modeli ya shimo jeusi kwa kutumia muongozo huu wa UNAWE ili kugundua zaidi kuhusiana na mashimo haya ya ajabu.

This Space Scoop is based on Press Releases from Chandra X-ray Observatory , ESO .
Chandra X-ray Observatory ESO

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi