Miji ya Mizimu Angani!
Julai 11, 2012

Galaxi ni kama miji ya nyota angani ambayo hivi karibuni wanaastronomia wamegundua galaxi mpya 12 zinazofanana na miji ya mizimu, kutokana na kutokuwa na nyota zinazoishi humo! Galaxi hizi ndogo ziitwazo galaxi nyeusi ‘dark galaxi’ hazina mwanga wa nyota wa kuzing’aza. Wanaastronomia walitegemea kuwapo kwa galaxi hizi nyeusi, kwa sababu ya mchango wake mkubwa katika kutengenezeka na kukua kwa galaxi katika historia ya ulimwengu. Lakini ni baada ya ugunduzi huu ndipo watu walipoweza kuziona.

Galaxi nyeusi zipo mbali sana katika ulimwengu na maada zake zinafikiriwa kusaidia katika kutengeneza nyota kubwa zinazotengeneza galaxi zinazoonekana leo, kama ilivyo kwa galaxi yetu ya njia maziwa “Milky Way Galaxy”. Ingawa maada zilizotumika katika kutengeneza galaxi hizi kubwa zimeshatumika lakini bado zinaweza kuonekana leo hii kutokana kuchunguza ulimwengu wa mbali ambapo tunaweza kuuangalia katika wakati uliopita! (Ili kujifunza zaidi kuhusu ni jinsi gani wanaanga wanaweza kuangalia katika wakati uliopita bofya hapa)


Lakini ni kwa jinsi gani wanaastronomia wanaweza kuangalia galaxi ambayo ina giza? (Fikiria kama unaangalia mshumaa katika chumba chenye giza, kisha uzime mwanga wa mshumaa kwa kuupuliza na sasa inakuwa ngumu kuupata mshumaa katika giza.) “njia rahisi ni kuangaza maada katika kiza” anaeleza Simon Lilly, mmoja kati ya wanaastronomia waliofanya uvumbuzi huu. Ambapo hii ni sababu kuu inayowafanya wanaastronomia waziangalie galaxi nyeusi pembezoni mwa galaxi zenye mwanga mkali sana ziitwazo ‘quasars’ ambazo nazo pia zipo mbali sana katika ulimwengu. Mwanga kutoka katika quasars hufanya galaxi nyeusi ziangazwe na zing’ae” amesema Simon.

Dokezo

Galaxi hizi nyeusi zinaweza kuwa ndogo ukilinganisha na galaxi tunazoziona leo, lakini bado zina gesi nyingi zaidi ya mara billion 1 ukilinganisha na Jua!

This Space Scoop is based on Press Releases from RAS , ESO .
RAS ESO

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi