Utaonekana Vipi Kijana Wakati Sio
Dis. 19, 2012
Kuna baadhi ya watu ambao huwa na muonekano mzuri hata wakiwa na miaka 90, wakati wengine huonekana wazee wakiwa na miaka 50. Hakuna uhusiano wa watu wanavyozeeka na miaka waliyokwisha ishi, ila jinsi wanavyoishi hauthiri kwa kiasi kikubwa. Kuvuta sigara, kunywa pombe na kula vyakula visivyofaa vinaweza kukufanya uonekane mzee zaidi na kuishi maisha mafupi. Kitu ambacho ni kweli hata kwa makundi ya nyota!
Kundi la nyota kama hili lililopo katika picha, ni kundi la nyota zilizosongamana sana kutokana na nguvu ya uvutano. Zimetengenezwa haraka sana, hivyo nyota hizi zilizaliwa karibu karibu sana. Nyota zilizopo katika picha hii ni baadhi ya nyota za zamani sana katika ulimwengu mzima. Zilitengenezwa katika miaka karibuni bilioni 13 iliyopita na ulimwengu wenyewe una miaka bilioni 13.7! Ambapo wanaastronomia wamegundua kitu cha ajabu sana kilichojificha katika moyo wa nyota hizi kubwa na nzee: nyota changa!
Ambapo wamegundua kuwa nyota hizi changa pia ni za zamani sana. Zimekuwa na bahati ya kuchomwa sindano na kuwa vijana kwa mara ya pili. Pale ambapo nyota mbili nzee zinapogongana na kutengeneza nyota mpya, maada huamishwa. Nyota moja inapata nishati zaidi toka kwa nyingine. Nyota hiyo huwa nzito, na nyota nzito huvutwa kuelekea katikati ya kundi la nyota. Nishati mpya iliyopata hufanya nyota hizi kung’aa zaidi na kuzifanya zionekane hazina mda mrefu. Siri imefichuliwa!
Dokezo
Makundi haya ya nyota zilizosongamana yalikuwa yakitawala galaxi yetu, wakati ule ilipotengenezwa na kulikuwa na maelfu ya makundi haya yanayozurura angani. Leo hii kuna karibu makundi 150 yaliyobakia! Hivyo ni bahati kwa baadhi ya makundi haya kupata maisha mapya.
This Space Scoop is based on a Press Release from
ESO
.
Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania
Picha
Chapisha
Bado una shauku? Jifunze zaidi...
Space Scoop ni nini?
Vumbua astronomia zaidi
Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga
Marafiki wa Space Scoop