Mzimu wa Nyota
Jan. 9, 2013

Kuna watu zaidi ya mamilioni Duniani kote wanaoamini katika mizimu, na wengine wanadiliki kusema kuwa wameiona kwa macho. Kwa sasa nawe unaweza kujiita ni mmoja wa watu hao! Picha yetu mpya inaonyesha nyota kubwa katika maisha yake baada ya kufa, na unaweza kusema ni mzimu wa nyota.

Nyota kubwa hufikia wakati hufa kutokana na kuishiwa nishati, ambapo matabaka ya nje hulipuliwa katika mlipuko mkubwa, na kiini husambaratika chenyewe. Matabaka ya nje yaliyolipuliwa huweza kutengeneza maumbo mazuri ya kupendeza (kama hili), na ni katika kiini ambapo huwa na matukio ya kupendeza zaidi. Picha hii iliyopigwa huko angani inaonyesha kiini cha nyoa kubwa iliyokufa baada ya kupitia makashi kashi ya milipuko wakati wa kufa kwake.

Wakati matabaka ya nje yanatupwa mbali, kiini nacho husambaratika chenyewe, na kutoa maada za kutosha zenye uwezo wa kutengeneza Jua kama letu, maada hizo hukandamizwa katika eneo dogo zaidi ya lile la mji wa wastani! Na baada ya hapo kiini kinaanza maisha mapya ya baada ya kufa na kuishi kama aina mpya ya nyota. Katika picha kiini kimezaliwa upya kama ‘pulsar’. Ambayo ni nyota inayojizungusha kwa spidi kali mno – haraka zaidi ya panga la helikopta! Wakati inazunguka inasababishwa maada kutupwa  nje,  unaweza kuona baadhi ya maada zimetupwa kwa juu katika picha?

Bonyeza hapa na uone jinsi pulsar zinavyofanya kazi!

Dokezo

Pulsars zina nguvu kubwa mno ya uvutano yenye wigo mpana. Kama ungesimama kwenye uso wake basi uzito wako unaweza kufikia kilo million mbili, mara bilioni zaidi ya uzito wako wa hapa Duniani!

This Space Scoop is based on a Press Release from Chandra X-ray Observatory .
Chandra X-ray Observatory

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi