MWANGA UMULIKAO KATIKA ANGA LA JUPITA
Dis. 1, 2017

Duniani kote watu hufurahia kutazama mafataki yanapolipuliwa, iwe Novemba 5, siku ya kutoa shukrani , mwakampya wa Kichina au Diwali.

Lakini asili hutupatia onyesho zuri zaidi la mwanga. Shukrani kwa nguvu za usumaku za sayari na milipuko mikubwa ya nishati katika Jua, tunapata “aurora”.

Aurora ni miale ya mwanga inayomeremeta ambayo hucheza cheza angani wakati wa usiku kukatiza ncha ya Kaskazini na Kusini. Huweza kuonekana katika baadhi ya sayari katika mfumo wetu wa Jua, na kuzipamba anga kwa rangi nyekundu, bluu, kijani na hata kwa miale ya x-rays. Picha inaonyesha  mionzi ya x-ray ya aurora ambayo imeonekana kwa mara ya kwanza, ikimulika ncha za Kaskazini na Kusini za sayari ya Jupita.

Hadi hivi karibuni, tulifikiri kuwa kitu chochote kinachoweza kuathiri nguvu ya usumaku katika sehemu moja ya sayari, kingeweza kuharibu nguvu ya usumaku katika sayari yote. Hili linaweza kueleza kwanini aurora katika ncha ya Kaskazini na Kusini huakisiana. Lakini, Jupita haifanyi kazi sambamba na kanuni hii- aurora katika Jupita zinatabia zinazotofautiana baina ya ncha zake.

Aurora katika ncha ya Kusini ya Jupita hutoa miale ya X-rays kila baada ya dakika  takribani 1, kama vile saa ifanyavyo. Wakati katika ncha ya Kaskazini huonekana kung’aa na kufifia bila mpangilio.

Wanaastronomia hawana uhakika hasa ni kipi kinachopelekea mabadiliko haya yasiyo ya kawaida, lakini hili ni jambo ambalo wanashauku ya kulitafutia ufumbuzi.

Wigo wa nguvu za usumaku zinazozunguka sayari, huzuia chembe chembe hatari kutoka kwenye Jua na nyota na hutunza angahewa kupotea katika anga la ulimwengu. Kadri ya jinsi tujuavyo, maisha katika sayari hayawezi kuwepo bila uwepo wa angahewa. Hivyo, kama tunaweza kuona aurora katika sayari zilizo nje ya mfumo wa Jua, itakuwa ni kiashiria cha uwezekano wa kuwepo maisha ya viumbe wengine kwenye sayari hizo.

Dokezo

Kila eneo ambapo aurora inapatikana katika Sayari ya Jupita inachukua eneo lililo karibu sawa na nusu ya uso wa Dunia!

This Space Scoop is based on a Press Release from Chandra X-ray Observatory .
Chandra X-ray Observatory

Kaweah, Gidion A. / UNAWE Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi