Kani ya uvutano: Nguvu Iliyoamka
Dis. 25, 2017
Huenda ushawahi kusikia msemo wa wahenga usemao “kilicho juu kingoje chini”, lakini je, ushawahi kukaa na kufikiri ni kwanini? Jibu lake ni “Kani ya uvutano (Gravity)”.
Kani ya uvutano ni kani isiyoonekana ambayo huvivuta vitu pamoja au kwa kuelekeana. Kitu chochote chenye uzito kina kani ya uvutano. Kitaalamu Uzito ni kiasi cha maada kinachobebwa katika kitu. Kadri ya kitu kinavyokuwa na uzito mkubwa, ndivyo kani yake ya uvutano pia huwa kubwa
Miongoni mwa vitu vyenye uzito mkubwa ulimwenguni ni makundi makubwa ya nyota (galaxies). Makundi haya ni makubwa sana na yana mabilioni ya nyota, sayari, mavumbi ya ulimwenguni na vitu vinginevyo.
Licha ya umbali mkubwa kati ya kundi nyota moja na jingine, nguvu ya uvutano baina yao bado ni maradufu. Hii huyafanya makundi nyota haya kuvutana pamoja na mara nyingi huishia kugongana.
Picha hii inaonesha kundi la nyota lenye rangi rangi.lakini lenye umbo lisilo maalumu. Upekee wa umbo lake ni kutokana na kuwepo makundi mawili ya nyota. Jozi hii ilitokana na kugongana kwa makundi nyota mawili mamilioni ya miaka iliyopita. Yalivutwa pamoja na kani ya uvutano, ambayo bado, inaendelea kuyaunganisha taratibu na kutengeneza kundi moja kubwa la nyota kubwa.
Karibu kila kundi nyota litapatwa na janga la kugongana na mengine katika muda fulani. Hii inaweza kumaanisha makundi mawili ya nyota yatagongana baina yao kama ilivyo katika picha, au yanaweza kupishana kidogo na kuruhusu kani ya uvutano iyafanye yawe na maumbo ya tofauti.
Dokezo
Kundi nyota letu .la Njia ya maziwa (The Milky Way Galaxy), linahistoria ndefu ya kugongana na makundi mengine. Lina makundi madogo mengi ya nyota ambayo yaliyogongana nalo vikundi katika miaka ya nyuma. Kwa hakika, hata hivi sasa kundi dogo la nyota lililo karibu na letu linaunganika na letu hivi sasa tunavyoongea.
Kaweah, Gidion Anderson / UNAWE TANZANIA
Picha
Chapisha
Bado una shauku? Jifunze zaidi...
Space Scoop ni nini?
Vumbua astronomia zaidi
Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga
Marafiki wa Space Scoop